Manager wa Diamond, Babu Tale amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar-Es-Salaam yeye ndiye anayejua alipo Msanii Roma na Wenzake waliotekwa juzi Jumatano jioni katika Studio za Tongwe Records Jijini Dar.
Babu Tale ametumia Mtandao wa Instagram Kuelezea hisia zake hizo kwa kupost Picha hii hapa chini ya Paul Makonda na Kusisindikiza na Maneno hayo hapo Chini ya Picha.
“Uoga ni uzembe me nazani mwenye jukumu la kujua Roma yupo wapi ni Mkuu wa koa sababu yeye ndio kiongozi wa kamati ya usalama ya mkoa sasa ikiwa tumezunguka vituo vyote vya polisi na mwenzetu atumuoni nani wa kumfuata kumwambia tunamtaka mwenzetu kama sio @paulmakonda me naanza hili bila uoga mkuu wa mkoa naomba utusaidie kutuambia mnzetu @roma2030 alipo. Tukutane Tongwe mida hii me nipo kwa foleni wakuu #uogauzembe#freeroma”
Kufuatia Post hiyo ya Babu Tale Watanzania wametoa Maoni yao mbali mbali unaweza kuyasoma kwa kufuatilia Post hiyo hapo chini ikiwa kwenye instagram moja kwa moja
