Hivi ndivyo Watanzania na Wakenya wanavyomlilia Roma ikiwa siku ya pili tangu atekwe

In Burudani

Inatanda Tanzia na hofu miyoni mwa Watanzania kufuatia kutekwa kwa wasanii wa Hi-Hop Nchini, Roma Mkatoliki na Moni Centrozon,  producer wa Tongwe Records, Bin Laden pamoja na Vijana wengine ambao walitekwa usiku wa Juzi jumatano majira ya Saa moja jioni ambapo Walipelekwa kusikojulikana na watu wasiojulikana.

Wasanii na watu maarufu wameendelea kulipigia kelel suala hili wakisisitiza Vyombo husika Serikalini kulifanyia utatuzi wa haraka suala hili lakini leo ni siku ya pili Wasanii hao hawajulikani walipo.

Jana Mke wa Roma, Bi Nancy amesema amezunguka katika vituo vingi vikubwa vya polisi kuulizia taarifa za mumewe jibu analokutana nalo ni “hatuna taarifa zozote, tutashughulikia.”

Nancy ameonekana kukosa tumaini kwa majibu hayo anayokutana nayo  na leo ni siku ya pili hamuoni wala kusikia sauti ya mumewe aliyemuuaga usiku wa juzi kuwa anaenda Tongwe Records, studio ambayo hurekodi nyimbo zake.

“Serikali, waandishi wa habari, Watanzania, yeyote aliyeona, aliyesikia, anayeweza kutusaidia Roma yuko wapi naombeni msaada wenu,” ni Maneno ya mke wa Roma, Nancy ambaye yeye na Roma wana mtoto mmoja wa kiume aitwaye Ivan.

“Nahitaji kufahamu yuko wapi, yuko katika hali gani,” ameongeza hayo kwa uchungu.

Hata hivyo RPC wa Kinondoni jana amesema hawana taarifa yoyote kuhusu kukamatwa kwa ROMA na watatoa taarifa baada ya masaa 48. Zaidi

Wasanii na watu Maarufu nchini wameonyesha kuingiwa Hofu kwa suala hili na haya ni baadhi ya Waliyoyaandika kwenye mitandao ya kijamii:-

Diamond

Wakati mwingine natafakari sijui hata wapi tunaelekea… lla kwakuwa Mwenyezi Mungu ndio Mpangaji wa yote basi naamini hata hili litapita tu… Mwenyezi Mungu aipe nguvu familia ya @roma2030 na wanamziki wenzetu wote ambao hadi sasa haijajulikana walipo..

Nay wa Mitego

Siku nzima ya leo nimekosa raha kabisa, cjui Mshkaji wangu Yupo kwenye hali gani, mazingira gani.? Roma yuko wapi.?! Sim yake ukipiga inaita Kama kawaidi, Masege Whatsup zinasomwa, Sim hazipokelewi. Vyombo husika tunaomba mtusaidie, tunaitaji kujua ndugu zetu wako wapi.? Hatuwezi kukaa kimya.
Hivi kweli tumefikia huku.? Tunaenda wapi.? #FreeRoma
#Wapo

Fid Q

Nimeipokea hii HABARI kwa mstuko mkubwa.. sio tu kwasababu TONGWE ni moja kati ya wadhamini wetu wa #OpenMicThursday pia ni moja kati ya studio ambazo zimekua msaada mkubwa sana ktk kunyanyua vipaji na C E O @j_murder_tongwe amekua mstari mbele sana ktk kufanikisha hilo.. kinachonistua na kuninyima raha zaidi ni hili la hawa ndugu zetu akina @roma2030 @moni_centrozone Producer Belo na mlinzi kuwa hawajulikani waliko hadi hivi sasa.. ninaiomba MAMLAKA HUSIKA ya USALAMA itusaidie ili waweze kupatikana mapema na kuifutilia mbali ile hofu iliyotanda mioyoni mwa ndugu, jamaa na marafiki… mwisho namuomba MUWEZA WA VYOTE azifanyie wepesi familia za ndugu zetu waliopotelea kusikojulikana in sha Allah

GNAKO

#Romayukowapi #moniyukowapi #producerbinladenyupowapi ???

Professor Jay

Wakati sisi tunakosa Usingizi na kuendelea kupaza Sauti, Kuna wengine wameweka miguu juu wanaona hili haliwahusu na wengine wanakwenda mbali zaidi na kudiriki kusema hii ni KICK ya Muziki tu..
Narudia tena kuwaambia ndugu zangu WAKIMALIZANA NA SISI WATAKUJA KUMALIZANA NA NYINYI
#Bring Back our SOLDIERS Alive.
NIKKI WA PILI

Kiongozi wa chama cha wasanii …… Tuma….. kushirikiana na wasanii tunatafuta taarifa juu ya swala hili…..

Vanessa Mdee

Wherever you are, God is Bigger than, Stronger than, Realer than all the other forces that be. Stay UP brother @roma2030 #VivaRoma #FreeRoma #FreeMoni roho inauma na nimetoka kumsikiliza mkeo redioni hajui hata ulipo sasa ndiyo nini ‘”?” “?” is this where we are at now? Ma studio yanavamiwa, watu wanakamatwa kama wanyama pori. Aaaarrrrgh


Ray C

Nimeanza kuingiwa na woga,nafikiria mambo mengi Roma alipo Sasa,anafanywa nini na tatizo ni nini mpaka imekuwa hivi na masaa yanaenda hakuna jibu lililo kamili!! hisia mchanganyiko na zote sio nzuri….Nini kinaendelea?Tatizo ni nini??Sababu ni nini?Bado najiuliza sipati jibu………

AY

Vyombo husika vifanye uchunguzi wa haraka tujue hali za wasanii wenzetu wako kwenye hali gani..@romamkatoliki Mungu yupo pamoja nanyi awaepushie lolote baya.. @tongwerecords @j_murder_tongwe

Zitto Kabwe Ruyagwa ‏  Verified account @zittokabwe

If we continue being silent on whereabouts of Ben Saanane we will have no moral authority to raise our voice on other whereabouts forward

Shilolekiuno_badgirlshishi

We all need to coorporate and save the life of this artist@roma2030

ALBERT MSANDO.

Ikifika kesho hatujui alipo @roma2030 ni marufuku kwa radio au TV yoyote kupiga muziki au nyimbo ya msanii wa Tanzania. Hatutaki. Kama @roma2030 ana kesi yakujibu apelekwe kwenye vyombo vya sheria. Hatutakubali uonevu au unyanyasaji wa aina yoyote. Tanzania ni yetu sote. Katika hili tutasimama pamoja. #FreeRoma. @aytanzania @mwanafa@professorjaytz @vanessamdee @juma_jux@johmakini_official @diamondplatnumz@shilolekiuno_badgirlshishi @officialshetta@linexsundaymjeda @ommydimpoz@gnakowarawara @nikkwapili@darassacmg @youngdaresalama@youngkillermsodokii @officialalikiba@lordeyesmweusi @dogojanjatz@soggydoggyanter @jidejaydee @mhtemba@chegechigunda

Kutoka Nchini Kenya Mtangazaji wa Citizen Radio/TV naye amepost hiki hapa chini:-

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu