Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema chama hicho kitaiweka hadharani Ilani yake mpya ya 2025-2030 ambayo itanadiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025.
Rais Samia amesema kuwa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mwaka huu imeandaliwa kwa ushirikiano mpana unaojumuisha wananchi, asasi za kiraia, na wadau mbalimbali wa maendeleo, hatua iliyolenga kuhakikisha ilani inaakisi mahitaji halisi ya wananchi na dira ya maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Rais Samia amesema kuwa Ilani hiyo itazinduliwa Ijumaa, Mei 30,2025.
Ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma,.



