CCM yamtolea nje Wema Sepetu.Yasema Haina Taarifa ya Yeye Kurudi

In Kitaifa, Siasa

Baada ya Muigizaji Wema Sepetu kutangaza kurudi ndani ya Chama Cha Mapinduzi baada ya kukihama Februari mwaka huu, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa chama hicho hakina taarifa yoyote ya kurudi kwa Wema Sepetu.

Polepole amesema CCM ina utaratibu wa mwanachama kujiunga na chama hicho na kuongeza kwamba chama chao siyo daladala kwamba mtu anaweza kupanda na kushuka wakati wowote apendao, na kwamba CCM ina misingi, imani na masharti ya uanachama.
“Kupitia utaratibu na muundo wetu wa chama kwenye shina kisha ataandikwa kwenye orodha ya wanachama kwenye tawi ambalo yeye ni mkaazi,” amesema Polepole.
Ameongeza kwamba habari za Muigizaji huyo kurudi ndani ya CCM yeye amepata taarifa mitandaoni kama jinsi watu wengine walivyozipata.
Pamoja na hayo polepole amefafanua kuwa “Ni heri abaki huko huko (Chadema) au akaanzie kule ambako alichukulia kadi yetu, Kuijenga CCM mpya yenye kuheshimu nidhamu ya chama siyo kazi ndogo na inataka viongozi wenye unyenyekevu, watumishi na wanachama wavumilivu. CCM mpya itakuwa chungu kwa baadhi yetu lakini tamu kwa wengi wetu”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu