Joshua Nassari avamiwa na watu wenye bunduki,waua Mbwa.

In Kitaifa

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amedai usiku wa kuamkia Jumamosi hii alivamiwa na watu wasiojulika wakiwa na bundiki na kufyetua risasi nje ya nyumba yake.

 

Nassari amedai muda mchache baada ya tukio hilo yeye pamoja na mke wake walifanikiwa kufika kituo cha polisi na kutoa ripoti na tukio hilo.

“Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya USA RIVER usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi. Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu,” alitweet Nassari.

Amedai watu hao baada ya kufyetua risasi walifanikiwa kumuuwa mbwa wake ambaye alikuwa nje ya nyumba.

Mbunge huyo mara kadhaa amekuwa akiripoti katika mitandao ya kijamii kwa amekuwa atishiwa kuuawa mara kwa mara.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu