China yagoma kukimega kisiwa cha Taiwan.

In Kimataifa

China imesema kamwe haitotoa hata inchi moja ya eneo lake, ikiwemo kisiwa cha Taiwan. Waziri wa Ulinzi wa China, Wei Fenghe amesema leo kuwa nchi hiyo haifikirii pia kuigawa sehemu yake katika Bahari ya China Kusini ambayo inazozaniwa.

Waziri huyo ameitoa kauli hiyo wakati akifungua kongamano la Xiangshan mjini Beijing.

Hivi karibuni China ilikasirishwa na vikwazo vya kijeshi vya Marekani, ikiwa ni moja ya mivutano katika uhusiano wake na Marekani, ikiwemo vita ya kibiashara na kuongezeka kwa uhasama wa kijeshi kati ya China na Taiwan katika Bahari ya China Kusini.

Wei amesema uhusiano wa kijeshi kati ya China na Marekani ni muhimu sana.

Wiki iliyopita, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Jim Mattis alimwambia Wei kwamba nchi hizo zinahitaji kuimarisha uhusiano wao ili kuondoa mvutano na kuzuia hatari ya kuzuka kwa mzozo usiotarajiwa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu