Ethiopia yapata Rais mwanamke kwa mara ya kwanza.

In Kimataifa

Bunge la Ethiopia limemuidhinisha Sahle-Work Zewde kuwa rais mpya na kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo. Sahle- Work anachukua wadhifa huo baada ya Mulatu Teshome Wirtu kujiuzulu jana Jumatano. Bi Sahle-Work amehudumu kama balozi wa Ethiopia katika mataifa ya Ufaransa, Senegal na Djibouti na pia katika jumuiya ya ushirikiano wa maendeleo wa nchi za Afrika Mashariki na pembe ya Afrika IGAD. Kabla ya kuteuliwa kuwa rais, alikuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa umoja huo kwa Umoja wa Afrika. Kama rais anatarajiwa kuhudumu mihula miwili ya miaka sita kila mmoja. Hayo yanakuja wiki moja tu baada ya Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kuteua asilimia hamsini ya wanawake kuhudumu katika baraza la mawaziri, na kuifanya nchi hiyo kuwa ya tatu barani Afrika baada ya Rwanda na Ushelisheli kuwa na usawa wa kijinsia katika baraza la mawaziri.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu