Crystal palace waliendeleza nia yao ya kutaka kusalia katika ligi kuu nchini uingereza huku wakiangamiza nia ya Arsenali ya kutaka kumaliza ligi hiyo katika nafasi nne bora kwa kuwatitiga, kuwavyoga na kuwanyeshea mvua ya magoli 3-0 jana usiku.
Palace walichukua uongozi mnamo dakika ya 17 kupitia mchezaji Andros Townsend kisha Yohan Cabaye akaongeza la pili mnamo dakika ya 63 naye luka Milivojevic akamaliza kazi mnamo dakika ya 68 kwa kupitia mkwaju wa penalty. Palace sasa wamechupa hadi nafasi ya 16 na pointi 34 kwenye jedwali la EPL huku watoto wa wenger wakikita kambi katika mtaa wa sita sasa na pointi 54 tatu nyuma ya nambari tano Manchester united.
