Justin Bieber Kutumbuiza Afrika

In Burudani
Muimbaji wa muziki kutoka Mkanada Justin Drew Bieber ‘Justin Bieber’ kutua tena kwa mara nyingine nchini Afrika Kusini kwa lengo la kufanya shows katika miji miwili tofauti.

Kwa mujibu wa ‘Purpose World Tour’ ya Justin Bieber ratiba inasema ataperform mijini Johannesburg jumapili ya tarehe 14 mwezi May katika eneo lililopangwa la viwanja vya FNB(FNB Stadium) kisha mjini Cape Town jumatano ya tarehe 17 mwezi May katika uwanja wa Cape Town(Cape Town Stadium).

Mara hii katika show hizo mbili za Afrika Kusini yametajwa mambo kadhaa muhimu ya kuzingatia ikiwa ni pamoja watoto wenye umri chini ya miaka 14 ni lazima wawe na mtu atakayekuwepo kwa uangalizi, na watoto wote wenye umri chini ya miaka 12 na wafupi kimo cha mita 1.2 hawataruhusiwa kuingia kushuhudia shows hizo.

Hata hivyo ujio huo wa Justin Bieber ni mara yake ya pili ambapo kwa mara kwanza ilikuwa ni mwaka 2013 show ambayo ilifana vilivyo ingawa inatazamiwa kuwa show hii ijayo itakuwa ya mafanikio makubwa zaidi kwakuwa Justin Bieber ameongeza mashabiki mara dufu.

Tour hii ya Justin Bieber ilioanza March 9, 2016 inategemewa kumalizika September 6, 2017 ambapo baada ya Afrika Kusini itaendela mjini Landgraaf, nchini Netherlands kisha mjini Aarhus, Denmark.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Tigo na mjasiriamali Boss yaja kukomboa wajasiriamali

Katika kuendelea kukuza utalii wa utamaduni hapa nchini kampuni ya Tigo kanda ya kaskazini imeendeleaa kuwaunga mkono wadau wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu