Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza mabadiliko ya bei za mafuta nchini zitakazoanza kutumika kuanzia leo, huku mafuta ya petroli yakionekana kushuka.
Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuya ya taa, zimebadilika ikilinganishwa na bei za Machi Mosi mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo katika Makao Makuu ya ofisi za EWURA, Meneja Mawasiliano ma Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo amesema, bei ya reja reja ya petroli imepungua kwa Shilingi tatu kwa lita ambayo ni sawa na asilimia 0.13, pianbei ya jumla imepungua kwa Shilingi 5.65 kwa lita sawa na asilimia 0.29.
Aidha Kaguo amesema bei ya rejareja ya Dizeli imepanda kwa Shilingi saba kwa lita sawa na asilimia 0.36 wakati bei ya jumla ikiwa imepanda kwa Shilingi 3.68 kwa lita sawa asilimia 0.21.
