Chama hicho kinachowakilisha ligi za Ulaya ambacho kina wanachama kutoka katika nchi 25 maarufu kama (EPFL), kimekua kikienda kinyume na kuipinga UEFA tangu kuachwa kushirikishwa kwenye mabadiliko ya maingizo kwenye klabu bingwa Ulaya na mgawanyo wa fedha za washindi.
Awali kulikuwa na makubaliano kati ya EPFL na UEFA juu ya kuepuka ligi kuingiliana yalimalizika muda wake mwezi uliopita, na EPFL wakasema ligi zake kwa sasa zitakuwa huru kuweka mechi katika muda unaofanana na ule wa klabu bingwa Ulaya na mechi za Europa League.

Rais wa UEFA Aleksander Ceferin
“Haiwezekani kufikiria na kuingia mtego wa ulaghai kutoka kwa wale wanaoamini kuwa wanaweza kuzizunguka na kuzitumia ligi ndogo katika kutaka kuweka adhima yao ndani ya mashirikisho kadhaa kwa sababu tu wanaamini wanaweza kufanya hivyo kutokana na nguvu wanayopata kutokana na mapato ambayo ligi za ndani za nchi zao zinaingiza,” Ceferin alisema kwenye mkutano wa UEFA mapema leo jijini Helsinki nchini Finland.
Rais wa FIFA Gianni Infantino alihudhuria mkutano huo na kusema kuwa uchaguzi uliomweka Ceferin madarakani mwaka jana ulimaliza uadui uliokuwepo katia ya UEFA na FIFA,Kwa kusema “Huu ni upinzani wa kipuuzi kati ya UEFA na FIFA ambao haupo tena na ambao hautakiwi kuwepo,”
Kwa muongo mmoja sasa shirikisho la Soka Duniani limekuwa likilaumu shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA kuwa linapoteza fedha nyingi kwa njia isiyojulikana hususani kwenye mapato kitu ambacho FIFA imekiita kama ufujaji wa pesa.
