Baada mkoa wa Tabora kufanya vizuri na kushika nafasi ya
kwanza kitaifa kwa 2019 katika zoezi la kugawa vitamburisho
vya wafanyabiashara wadogo,mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri ameanza ziara ya kuhamasisha kundi hilo kuchukua
vitamburisho hivyo.
Akiwa wilayani Nzega RC Mwanri amewataka wafanyabiashara
wadogo ambao hawana vitambulisho hivyo kuchangamkia zoezi
hilo ili kuepuka usumbufu hapo baadae.
