Kama unakumbukumbu juzi kati nilikupa tarifa ya Aliyekuwa Mchumba wa CB Karrueche kufikisha shauri lake Mahakamani kwamba CB anamsumbua na Kumpa Vitisho.
Kwenye shauri lake Karrueche alisema kwamba CB bado anaingilia maisha yake na kumtishia kwamba endapo atamkuta na mwanaume atamfua yeye na huyo mwanaume na Shauri hilo lilitolewa Kauli na Hakimu la kumtaka Chriss Brown kukaa mbali na Karrueche.
Baada ya siku 2 nilikupa taarifa tena kwamba Marafiki wa karibu na CB wamesema kwamba CB anapitia wakati mgumu sana wa kutumia madawa ya kulevya kupita kiasi kwa sababu ya maumivu ya mapenzi aliyonayo na sasa hivi kuna time anafanya vitu vya ajabu mpaka wao wanamuonea huruma huku wakiongeza zaidi kwamba sbb ni kwamba CB bado anampenda Karrueche na anatamani kurudiana naye ila mwanadada huyo amekuwa akimchana CB kwamba hamtaki tena.
Sasa wakati hayo yakiendelea kuitafuna akili ya CB taarifa mpya ni kwamba hatimaye Karrueche amefumaniwa na Penzi lake la Siri.
Karrueche amedakwa na Camera za TMZ akiwa out na Mpenzi wake Mpya ambaye ni Quavo kutoka kundi la Migos.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja kilichozungumza na TMZ, wawili hao wamekuwa wakionekana sehemu tofauti tofauti pamoja kwa miezi michache sasa.
Kinachoongeza Asilimia za kuamini hilo ni kwamba Karrueche alionekana Biloxi wikiendi iliyopita katika tamasha la Migos.
