Baraza la usalama la umoja wa mataifa, limepiga kura kwa kauli moja kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini, kama adhabu ya kufanyia majaribio zana zake za nyuklia.
Vikwazo hivyo vinalenga kuhujumu uwezo wa Pyongyang, kufadhili na kutoa tawi kwa mpango wake wa nyuklya.
Vikwazo hivyo pia vinatoa masharti kwa biashara ya kununua mafuta ya Korea Kaskazini, mbali na kupiga marufuku uuzaji wa nguo katika mataifa ya kigeni.
Taarifa ya chombo cha habari cha Korea Kaskazini KNCA imeonya kwamba, iwapo Marekani itasisitiza vikwazo vikali dhidi ya taifa hilo, Korea Kasakzini itahakikisha kuwa Marekani inagharamikia hilo.
