Mbunge: Juma Nkamia aichana Serikali kuhusu suala la Kutekwa Roma na Wenzake

In Kitaifa

Mbunge wa Chemba Juma Nkamia Jumanne hii alipata nafasi ya kusimama Bungeni Dodoma katika kuchangia maoni kuhusu mapitio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri mkuu na ofisi ya bunge kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Katika vitu alivyoongelea Nkamia ni kitendo cha Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr. Harrison Mwakyembe kwenda katika mkutano wa msanii Roma Mkatoliki alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana.

“Jana nilipata nafasi ya kuangalia Press Conference ya Roma. Najiuliza, Waziri wa habari alienda kufanya nini? Akiambiwa ndo alimteka Roma atakataa?,” aliuliza Mkamia.

“Mtu alitekwa, serikali ndo inamwandalia press conference na kuisimamia? Ivi kesho mkiambiwa ndo mlihusika kumteka mtakataa? Najua ukweli unauma, lakini lazima tuseme. Serikali wakati mwingine mnaingia kwenye mitego wenyewe na mnamgombanisha Rais na wananchi.Nimesema ukweli, wengine wataanza kuwaza labda ni kwa sababu nilikosa uwaziri…..No, lazima tuseme ukweli.” aliongeza.

Roma pamoja na wezake wawatu walikutana na waandishi wa habari kueleza kichowakuta baada ya kutekwa na watu wasiojulikana.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu