KENYA: Wanajeshi wa KDF wamewauwa wanamgambo 15 wa Al shabaab usiku wa kuamakia jana wakati walipovamia kambi yao ya Katamaa umbali wa kilomita 100 kutoka mpaka wa Kenya na Somalia katika mji wa Elwark.
Akiongea na waandishi wa Habari, msemaji wa jeshi la KDF kanali Joseph Owuoth ameelezea kuwa wanajeshi walifanikiwa kuvamia na kuharibu kambi iliyokuwa na magaidi hao kwa kutumia mizinga waliyo kuwa nayo.
Aidha joseph amewahakikishia wakenya kuwa serikali itaendelea kushirikiana na jeshi la Somalia ili kupambana na magaidi huku akisema tayari hali ya kawaida imerudi katika miji kaadha nchini Somalia ikiwemo mji wa kismayu.
Inaaminika kuwa baadhi ya wanamgambo walifanikiwa kutoroka wakiwa na majeraha huku wanajeshi wa KDF wakiwa wapo salama na hakuna anaye uguza jeraha lolote.
