Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama, amesema mishahara
ya watumishi wa umma itapanda ifikapofika Julai 2022 ambapo
sasa wizara imeanza kupitia taarifa za Watumishi katika Mfumo
wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara
Waziri Mhagama amesema ofisi yake imejipanga kupandisha
mishahara ya watumishi wa umma kwa wakati kama
alivyoelekeza Rais Samia wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Wafanyakazi Duniani
Amesema ofisi yake itafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha
ifikapo Julai 2022 kila mtumishi wa umma anapata mshahara
mpya.
Hivyo amewataka watumishi wa umma kuwa watulivu wakati
zoezi hili likiendelea kushughulikiwa na Serikali.



