Mkali wa Muziki wa Country Don Williams afariki Dunia.

In Burudani, Kimataifa

Mwanamuziki nyota wa nyimbo za mtindo wa country kutoka Marekani Don Williams amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78.

Mzaliwa huyo wa jimbo la Texas amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi, afisa anayesimamia mawasiliano yake ametangaza.

Williams alianza kuimba nyimbo kama mwanamuziki wa kujitegemea mwaka 1971, na tangu wakati huo alichomoa nyimbo 17 zilizogonga chati za muziki wa country.

Nyimbo zake zilizovuma zaidi ni pamoja na Gypsy Woman na Tulsa Time, ambazo ziliimbwa tena na wanamuziki wengine kama vile Eric Clapton na Pete Townshend. Williams alitazamwa na wengi kama gwiji mnyenyekevu wa muziki wa country.

Nyimbo zake nyingine zilizovuma ni pamoja na You’re My Best Friend, I Believe in You na Lord, I Hope This Day Is Good.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Serikali kuunga mkono juhudi za Taasisi mbali mbali.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi, amesema serikaliitaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi yaZanzibar Maisha Bora Foundation,pamoja na

Read More...

DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

Watanzania waendelea kunufaika Sekta ya Madini, ajira 15,341 zamwagwa, manunuzi ya ndani ya nchi yafikia Dola za Marekani bilioni

Read More...

MAFURIKO YAUWA 190 MALAWI

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Mafuriko ya Tropiki Freddy kulikumba eneo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu