Mrisho Gambo agawa vifaa vya kujikinga na (COVID-19)kwa madereva daladala

In Uncategorized

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo amegawa vifaa maalumu vya kujikinga na virusi vya Corona kwa madereva wa daladala kuwapaka abiria wakati wa kuingia kwenye magar yao
Akizungumza na vyombo vya habari mwenyekiti wa umoja wa daladala mkoani Arusha Bila Albaro amesema vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya kujikinga na corona ambapo mkoa wa Arusha umetoa ndoo, na vitakasa mikono kwa madereva daladala kunawa mikono na abiria


Amesema kuwa, zoezi hilo lianza rasmi leo katika stand ya daladala Kilombero ambapo litakuwa endelevu huku wakiendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa madereva n makondakta kwa hii itasaidia kwa kiwango kikubwa kuepuka maambukizi ya corona Zoezi hili niendelevu wala halina mwisho hadi kujua muhafaka wa virusi hivi na standi zote zoezi hili zinafanyika ambapo tutashirikiana na jeshi la polisi ili kuhakikisha kila dereva anatumia vifaa hivyo ipasavyo kwa kuzingatia maagizo ya serikali  na wataalamu wa afya. amesema mwenyekiti huyo


Kwa upande wake katibu wa chama cha Daladala mkoani Arusha AKIBOA Bw.  Said Sharifu amesma kuwa licha ya msaada huo kutolewa lakini bado kuna changamoto ya watu kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na kujikinga na watu wanakuwa wabishi unawa mikono yao hivyo akawataka wananchi kufuata maagizo yanayotolewa na wataalamu wa afya ili kuepukana na janga hili
Sharifu amesema kuwa, anampongeza mkuu wa Mkoa na wadau wengine wa maendeleo kuendelea kujitokeza kutoa misaada mbalimbali huku wakitoa elimu ya kutosha na kuwataka abiria kuacha ubishi na kunawa mikono kwa maji yanayotiririka, kuosha mikona na vitakasa mikono, na kukaa umbali ya mita moja ili kujikinga na virusi hivyo

Nao baadhi ya abiria ba madereva kutoka maeneo mbalimbali jijini Arusha wamejitokeza kupata vifaa hivyo huku wakioomba serikali kiendelea kuhamasisha ba kutoa elimu huku wakiahidi kuvifanyia kazi ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuwapaka abiria 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu