Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo amegawa vifaa maalumu vya kujikinga na virusi vya Corona kwa madereva wa daladala kuwapaka abiria wakati wa kuingia kwenye magar yao
Akizungumza na vyombo vya habari mwenyekiti wa umoja wa daladala mkoani Arusha Bila Albaro amesema vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya kujikinga na corona ambapo mkoa wa Arusha umetoa ndoo, na vitakasa mikono kwa madereva daladala kunawa mikono na abiria
Amesema kuwa, zoezi hilo lianza rasmi leo katika stand ya daladala Kilombero ambapo litakuwa endelevu huku wakiendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa madereva n makondakta kwa hii itasaidia kwa kiwango kikubwa kuepuka maambukizi ya corona Zoezi hili niendelevu wala halina mwisho hadi kujua muhafaka wa virusi hivi na standi zote zoezi hili zinafanyika ambapo tutashirikiana na jeshi la polisi ili kuhakikisha kila dereva anatumia vifaa hivyo ipasavyo kwa kuzingatia maagizo ya serikali na wataalamu wa afya. amesema mwenyekiti huyo
Kwa upande wake katibu wa chama cha Daladala mkoani Arusha AKIBOA Bw. Said Sharifu amesma kuwa licha ya msaada huo kutolewa lakini bado kuna changamoto ya watu kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na kujikinga na watu wanakuwa wabishi unawa mikono yao hivyo akawataka wananchi kufuata maagizo yanayotolewa na wataalamu wa afya ili kuepukana na janga hili
Sharifu amesema kuwa, anampongeza mkuu wa Mkoa na wadau wengine wa maendeleo kuendelea kujitokeza kutoa misaada mbalimbali huku wakitoa elimu ya kutosha na kuwataka abiria kuacha ubishi na kunawa mikono kwa maji yanayotiririka, kuosha mikona na vitakasa mikono, na kukaa umbali ya mita moja ili kujikinga na virusi hivyo
Nao baadhi ya abiria ba madereva kutoka maeneo mbalimbali jijini Arusha wamejitokeza kupata vifaa hivyo huku wakioomba serikali kiendelea kuhamasisha ba kutoa elimu huku wakiahidi kuvifanyia kazi ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuwapaka abiria



