Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limethibitisha kutokea kwa
tukio la mtoto mchanga kutupwa katika mtaro kwenye mtaa wa
Taufiq kata ya Viwandani anayekadiriwa kuwa na siku moja.
Akithibitisha taarifa hizo leo Kamanda wa polisi Martin Otieno
amesema mtoto huyu amekwisha kufariki na mama aliyefanya
tukio hilo amekatwa.
