Nyalandu aomba kumsafirisha Tundu Lissu Marekani kwa Matibabu Zaidi.

In Afya, Kitaifa

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameungana na viongozi wa Chadema kuweka kambi jijini Nairobi akisubiri ridhaa ya madaktari wa hospitali ya Nairobi kumpeleka Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu nchini Marekani kupata matibabu zaidi.

Nyalandu ambaye alifanikiwa kumuona Lissu na kuelezea hali yake, amesema kuwa madaktari wa hospitali ya Nairobi wamekuwa wazito kutoa ripoti maalum ya matibabu ya Lissu ili kumruhusu kumpeleka Marekani.

Mbunge huyo wa CCM ambaye amekuwa msitari wa mbele kushiriki kampeni ya kuchangisha fedha za kugharamia matibabu ya Lissu, ameonesha kuwa yeye ni mmoja kati ya watakaomsafirisha Lissu kwenda Marekani kupata huduma bora zaidi za matibau.

 “Tumekuwa #NairobiHospital tukisubiri MADAKTARI watoe RIPOTI ya mwenendo wa MATIBABU ya Mh #TunduLissu kwa minajili ya kuwapatia MADAKTARI BINGWA wa Marekani na kuona uwezekano wa Mh #TunduLissu kupatiwa RUFAA kwa matibabu zaidi NJE., LAKINI bado KALAMU zao ni nzito kuandika RIPOTI hii siku ya tatu tangu tuahidiwe. Binafsi, nimerudi NAIROBI tangu JANA kushiriki maandalizi ya uwezekano wa kumhamishia Mh #TunduLissu Marekani kwa ajili ya huduma yenye ubora zaidi, endapo MADAKTARI wa #NairobiHospital wangeridhia. Kesho asubuhi nitarejea hospitalini kusikiliza kauli ya mwisho ya MADAKTARI kuhusu RIPOTI hiyo.” Nyalandu ameandika Facebook

Lissu alijeruhiwa kwa risasi tano kati ya risasi zaidi ya thelathini alizoshambuliwa alipokuwa nyumbani kwake eneo la Area D mjini Dodoma, muda mfupi baada ya kutoka bungeni.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu