RAIS John Magufuli amewahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Shirikisho la Taifa la Utengenezaji wa Mitambo ya Viwanda la China (CNMIF) kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itawapa ushirikiano wa kutosha katika mpango wao wa kuwekeza katika uzalishaji wa nishati ya umeme, viwanda na kilimo nchini.

In Kitaifa

RAIS John Magufuli amewahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Shirikisho la Taifa la Utengenezaji wa Mitambo ya Viwanda la China (CNMIF) kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itawapa ushirikiano wa kutosha katika mpango wao wa kuwekeza katika uzalishaji wa nishati ya umeme, viwanda na kilimo nchini.

Dk Magufuli alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa CNMIF na Mbunge wa Bunge la Wananchi wa China, Zhan Xin.

Rais Magufuli alisema Tanzania imejiwekea malengo ya kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka megawati kati ya 1,500 na 1,800 zinazozalishwa hivi sasa hadi kufikia megawati 10,000 na ili kufikia malengo hayo, wawekezaji wanakaribishwa kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo vilivyopo kama vile gesi, makaa ya mawe na jua.

Wakati huo huo, Rais John Magufuli jana alikutana na Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak na viongozi hao walizungumzia utekelezaji wa mambo mbalimbali ya ushirikiano na miradi ya maendeleo iliyotokana na makubaliano ya mkutano wa wafanyabishara wa Tanzania na Ufaransa uliofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Rais Magufuli jana alikutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Uturuki nchini, Yunus Belet na Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Korea, Songwon Shin.

 

 

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Serikali kuunga mkono juhudi za Taasisi mbali mbali.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi, amesema serikaliitaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi yaZanzibar Maisha Bora Foundation,pamoja na

Read More...

DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

Watanzania waendelea kunufaika Sekta ya Madini, ajira 15,341 zamwagwa, manunuzi ya ndani ya nchi yafikia Dola za Marekani bilioni

Read More...

MAFURIKO YAUWA 190 MALAWI

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Mafuriko ya Tropiki Freddy kulikumba eneo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu