Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amemtaka Waziri wa Nishati na Madini Prof.Sospeter Muhongo, ajithamini na achie ngazi kwa kushindwa kusimamia wizara yake ya Nishati na Madini
Pia Rais Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa mamlaka ya TMAA pamoja na kuivunja bodi hiyo na kutaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachunguza wafanyakazi wa wizara ya Nishati na Madini kuangalia kama wanahusika katika kuwafumbia macho katika usafirishwaji wa mchanga huo
