Rais Museven atangaza (LOCKDOWN) dhidi ya Ugonjwa wa Ebola

In Kimataifa

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa amri ya watu kutotoka nje ya wilaya mbili ambazo mlipuko wa virusi vya Ebola ulianzia, kwa muda wa siku 21, akisema kwamba serikali inafanikiwa kudhibithi maambukizi ya ebola nchini humo.

Amri hiyo itatekelezwa kadi Desemba tarehe 17.

Awali kulikuwa na amri kama hiyo ya siku 21 kuanzia Oct 15, na ilimalizika Nov 5.

Museveni amesema kwamba hatua hiyo imechukuliwa ili kuhakikisha kwamba mafanikio ambayo yamepatikana kufikia sasa katika kukabiliana na mlipuko wa Ebola, yanaendelea na kuhakikisha kwamba hakuna kabisa maambukizi ya virusi hivyo nchini humo katika muda wa siku chache.

Serikali imesema kwamba hakuna maambukizi mapya yameripotiwa katika wilaya hizo mbili

Watu 141 wamethibitishwa kuambukizwa Ebola nchini Uganda. 55 wamefariki tangu Septemba 20 mlipuko uliporipotiwa.

Hakuna chanjo dhidi ya virusi vya Ebola aina ya Sudan vinavyoripotiwa Uganda.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu