Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametangaza kuongeza kwa siku thelathini hatua za vizuizi vya kutoka nje kutokana na janga la virusi vya corona.
Maduro aliweka vizuizi vya kwanza mnamo Machi 13 na awali aliwahi kuongeza vizuizi hivyo hadi katikati ya mwezi Aprili.
Rais huyo wa kisosholisti amesema visa 423 vimeripotiwa huku watu kumi wakiaga dunia.
Ila idadi hiyo imetiliwa shaka na mpinzani wake Juan Guaido anayesema idadi ya walioambukizwa na kufariki iko juu mno kuliko ilivyotangazwa kutokana na kuanguka kwa mfumo wa afya nchini humo kutokana na miaka ya mzozo wa kiuchumi.
Masharti ya vikwazo hivyo ni kwamba mtu anaweza kutoka nje tu iwapo anakwenda hospitali au kununua chakula.
Venezuela pia imetangaza kurefusha hadi Juni 12 ndege kuingia na kutoka nchini humo
