RC MAKALLA AKUTANA NA BABA ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI ARUSHA

In Kitaifa

. Rc Makalla aomba Kanisa na viongozi wa dini zote kuendelea kuiombea nchi Amani na utulivu

. Askofu Isaac Amani aeleza umuhimu wa watanzania kuishi kwa Amani wakikumbuka wimbo wa Taifa kama sala kwa Nchi yetu

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Jumatatu Machi 30, 2026 amekutana na kuzungumza na Askofu Mkuu Baba Isaac Amani wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, akisisitiza umuhimu wa Viongozi wa dini katika maendeleo na ustawi wa jamii na kuahidi kushirikiana na Kanisa katika maendeleo ya Mkoa wa Arusha.

Mhe. Makalla amefika katika Kanisa kuu la Katoliki la Arusha kwa lengo la kujitambulisha kwa Baba Askofu Amani kama ilivyo utaratibu wake kwa Viongozi wa dini Mkoani hapa, akiliomba Kanisa pia kuendelea kuliombea Taifa amani na utulivu pamoja na kushauri mambo muhimu kwaajili ya Tanzania, akieleza utayari wake wa kupokea ushauri na busara kutoka kwa Viongozi wa dini kama sehemu muhimu ya kuuongoza Mkoa wa Arusha.

“Kila mahali nilipofanya kazi ninaona umuhimu wa kufanya kazi na Viongozi wa Kanisa; kubwa zaidi tuendelee kuiomba nchi yetu amani na utulivu kwani ninyi mnayo nafasi kubwa ya kuendeleza umoja na mshikamano katika nchi yetu, mtushauri na tunahitaji pia busara zenu ili tuendelee kukaa kama Watanzania kwa umoja.” Amesema Mhe. Makalla.

Kwa upande wake Askofu Amani amemshukuru Mhe. Makalla kwa kumtembelea na kuahidi kushirikiana na Serikali ya Mkoa katika kukuza ustawi na maendeleo ya Mkoa wa Arusha, akitoa rai kwa Watanzania kuuishi wimbo ww Taifa kikamilifu na kutafakari kwa kina maneno yaliyo kwenye wimbo huo kama sehemu muhimu ya sala kwa mwenyenzi Mungu ili aendelee kuilinda Tanzania.

Aidha Mhe. Makalla ametumia kikao hicho pia kumtakia Baba Askofu Amani pamoja na wananchi wote wa Mkoa wa Arusha sikukuu njema za Pasaka huku Baba Askofu Amani pia akiongoza sala ya kumuombea kheri na afya njema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Makalla pamoja na kuliombea Taifa amani na utulivu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TUMUOMBEE RAIS, TULIOMBEE TAIFA-MASHILI

Na Mwandishi Wetu, Tabora.WATANZANIA wamehamasishwa kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili

Read More...

JCB Ailipua Media, “Hip Hop Inabaniwa Redioni, Wasanii Wachache Wapewa Nguvu Zote!”

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, JCB, anayetoka kundi la Watengwa, ameeleza wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa

Read More...

Dkt Samia: Napunguza msafara wangu kupunguza matumizi ya mafuta

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ametangaza mpango wa kupunguza ukubwa wa msafara wake, ikiwa ni hatua za mwanzo za

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu