Rio Ferdinand kujiunga na ndondi baada ya kustaafu.

In Kimataifa, Michezo

Rio Ferdinand anazindua taaluma yake mpya kama mwanandondi miaka miwili baada ya kustaafu kutoka soka.

Hatua ya Rio mwenye umri miaka 38 kujiunga na ndondi imeiungwa mkono na kampuni ya kamari ya Betfair ambayo ilitangaza taraifa hizo leo Jumanne.

Mlinzi huyo wa zamani wa England na Manchester United pia ana kampuni yake ya nguo.

“Ninafanya hivi kwa sababu ni changamoto,” alisema Rio.” Nimeshinda mataji na sasa ninalenga kushinda mkanda.”

Amechapisha video kadha katika mitandao ya kijamii miezi ya hivi karibuni zinazomuanyesha akirusha ngumi na kupata mafunzo.

Aliyekuwa nahodha ya kikosi cha kriketi cha England Andrew Flintoff, pia naye alizindua taalumaa ya ndondi baada ya kustaafu, alipata ushindi mwaka 2012 dhidi ya Mmarekani Richard Dawson kwa pointi.

Ni kampuni ya Betfair iliyomuomba Ferdinand kuanzisha taaluma hiyo na itamsaidia kufuzu na kupata leseni ya bodi ya ndondi ya Uingereza kabla ya kuanza kujifunza na kushindana.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu