Serikali yatoa wito kwenye mifuko yote ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.

In Kitaifa

SERIKALI Imetoa Wito kwenye mifuko  yote ya uwezeshaji wa  wananchi kiuchumi  kuhakikisha wanapitia upya viwango vya Riba katika mikopo ambayo wamekuwa  wakiitoka wa wananchi kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini.

Wito huo umetolewa na waziri wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania KASIMU MAJALIWA kwenye uzinduzi wa wa maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji kwa wananchi kiuchumi ambayo yanafanyika mjini Dodoma.

Waziri MAJALIWA amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakiogopa kukopa katika mifuko hiyo kutokana na kuwa na liba kubwa ingawa wanapenda kukopa ili waweze kujikomboa  kiuchumi pia ameeleza kutokana na liba hiyo wanaona watashindwa kurejesha mkopo na mwisho wake watauziwa nyumba zao .

Hata hivyo amesema kuwa kila mfuko wa uwezeshaji kwa wananchi kiuchumi ianze kujitangaza pamoja na kujipambanua katika kazi zake ambazo wanazifanya na kwa ile mifuko ambayo bado awajafikia hatua hiyo na wao waanze kujipambanua kama mifuko mingine.
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza  uwezeshaji kwa wananchi kiuchumi Taifa JOHN JINGU amesema kuwa watahakikisha kila mfuko hiyo  inakuwa na kiwanda katika sehemu zao ambazo wanafanyia kazi  pia amesema kwa kufanya hivyo wataweza kuondokana na tatizo la ajira kwa vijana hapa Nchini.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKAGUA BARABARA YA SOMANGA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asubuhi ya leo  Aprili 16, 2025 amewasili eneo la Somanga kukagua Miundombinu ya barabara kuu

Read More...

HATUTAWAACHIA CCM NAFASI TUTASHIRIKI UCHAGUZI MKUU – ACT WAZALENDO

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amesema chama hicho kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka

Read More...

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamohanga Afariki Dunia 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Gissima Nyamohanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu