Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema sheria ya manunuzi
ya umma haijaweka kikwazo kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD)
kununua dawa moja kwa moja kutoka viwandani au kwa
wazalishaji ili kushusha gharama za dawa.
Waziri Ummy amesema sheria hiyo imeweka mipaka sio tu
gharama bali itaangalia ubora,ufanisi na upatikanaji wa dawa na
kwamba utaratibu wa kununua dawa moja kwa moja
umepunguza kwa kiasi kikubwa gharama za dawa nchini.
Ameeleza hayo jana bungeni jijini Dodoma,wakati akichangia
mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka
2022/2023 uliohitimishwa jana.



