Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai Mapema leo amewataka Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe kupitia CHADEMA Halima Mdee akiwa na Pingu.
Spika alitaja kosa linalomkabili Mbunge huyo kwamba ni Utovu wa Nidhamu uliopitiliza ambapo juzi April 4 mwak huu 2017 alitoa Lugha chafu za matusi kwa Spika wa Bunge wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Kwa upande mwingine Spika amemtaka pia Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kufika mwenyewe katika kamati ya maadili, kinga na madaraka ya Bunge siku ya leo kwa ajili ya kujibu tuhuma za kulidhalilisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

ZAIDI SIKILIZA HAPA CHINI
