Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imeanzisha huduma mpya ya uchunguzi kwa wajawazito ya magonjwa ya moyo kwa watoto, ambayo itasaidia kuokoa vifo vya watoto 120 hadi 240 wanaopoteza maisha kila mwaka.
Huduma hiyo ambayo ni ya kwanza kufanyika nchini kwa nchi za Afrika Mashariki, pia itawezesha watoto zaidi ya elfu 12 hadi elfu 13 wanaozaliwa kwa mwaka wakiwa na matatizo hayo, kupata matibabu mapema.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto Dk Naiz Majani amesema kuwa, kwa wastani mtoto mmoja kati ya 100 wanaozaliwa huwa na tatizo hilo.
