TAKUKURU YAJIPANGA KUKABILIANA NA RUSHWA KWENYE UCHAGUZI

In Kitaifa

DODOMA

Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania unaotarajiwa kufanyika July 19,2020, Taasisi ya kuzua na kupambana na Rushwa (TAKUKURU),Mkoa wa Dodoma imesema imejipanga vyema kukabiliana na vitendo vyovyote ambavyo ni kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 ya 2007.

Hayo yanajiri baada ya TAKUKURU Mkoani hapa kupataa taarifa za uwepo wa viashairia vya vitendo vya Rushwa kuelekea uchaguzi Mkuu huo.

Akizungumza leo na waandishi wa Habari Mkuu wa TAKUKU Mkoani Dodoma Bwana Sosthenes Kibwengo amesema wamebaini kuwepo kwa baadhi ya wagombea ambao wanatumia ushawishi wa fedha kwa kuwalipia ada za uanachama wafugaji ili wapate sifa za kupiga kura.

Amesema kwa kutumia utaratibu huo ni wazi kuwa inaashiria vitendo vya rushwa ili wao au wagombea wanaowaunga mkono wapigiwe kura, na kwamba wapinzani wao au wagombea wasiowaunga mkono wasiweze kuchaguliwa.

‘’Tunafuatilia nyendo za watu hao na tatachukua hatua stahiki baada ya kujiridhisha kwa uwepo wa ushahidi kwa wote wanaojihusisha na vitendo hivyo’’

Wakati huo huo amewasihi wafugaji wote kutoa taarifa za vitendo hivyo ili kuhakikisha kuwa uchaguzi wa viongozi wa chama cha wafugaji nchini unakuwa wa huru na wa haki kwa mujibu wa katiba, kanuni na miongozo ya chama cha wafugaji Tanzania na sheria za nchi.

‘’Taarifa kuhusu vitendo vya rushwa wakati wa kampeni na kuekekea siku ya uchaguzi wa viongozi wa chama cha wafugaji ya kitaifa ziwasilishwe kupitia simu ya bure namba 113 au kwa kufika kwenye Ofisi za TAKUKURU.

Katika hatua nyingine TAKUKURU Mkoani hapa imefanikiwa kuwafikisha mahakama ya wilaya ya kondoa watu sita ambao wameshitakiwa kwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15(1) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007.

‘’Mshitakiwa wa kwanza katika shauri hilo la jinai namba 41/2020 ni Pendo Boniface Machoke (28) ni afisa mtendaji wa kijiji cha Porobanguma, Affa Salim Maulid (37), Maulid Juma Iddi (48), Raphael Andrew Mrata (45),Ramadhan Hassan Mkaro (62) na Bakari Juma Aluu (65)’’.

Washitakiwa wote ni wajumbe wa Halmashauri ya kijiji cha Porobanguma kilichopo kata ya kwamtoro wilaya ya chemba na wanadaiwa kupatikana na kosa la kuomba rushwa ya shilingi milioni moja (1,000,000) kwa mwananchi mmoja ili wasimpeleke polisi kwa tuhuma za kubadili namba ya stakabadhi iliyotolewa na Halmashauri ya wilaya ya chemba.

TAKUKURU pia imewatia hatiani Bwana Venance Manyungwi Mwenyekiti wa kijiji cha Bahi Makulu na Bwana Jumanne Mbezi aliyekuwa Askari wa Jeshi la akiba kwa kosala kuomba na kupojea rushwa kinyume na kifungu cha 15(1) cha sheria za kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11/2007 katika shauri la jinai namba 32/2018.

‘’Mayungi amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000) na Mbezi amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya shilingi milioni mbili na laki tano (2,500,000) na walifikishwa mahakamni baada uchunguzi kuonyesha kwamba waliwakamata wananchi kadhaa wa kitongoji cha Suguta B na kuwasingizia wamehusika na mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji hicho hivyo kuwataka watoe fedha ili wasipelekewe polisi’’ Kibwengo

Amesema’’ mahakama imeridhishwa na ushahidi uliowasilishwa ambao umethibitisha wawili hao kupokea hongo ya shilingi 730,000 kutoka kwa wanachi waliowakamata,mshitakiwa Bwana Mbezi amehukumiwa bila kuwepo mahakamani hapo kwani alitoroka baada ya kuruka dhamana’’ Kibwengo

Hata hivyo, Wananchi wameeendelea kukumbushwa kuwa mapambano dhidi ya Rushwa ni ya wote hivyo waendelee kushirikiana vyema ili kuhakikisha kuwa wote wenye mamlaka wanatumia nafasi zao kulingana na Sheria na kanuni za nchi na si kwa maslahi binafsi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu