Tetesi za Soka Ulaya leo Jumatano Septemba 22, 2021

In Kimataifa, Michezo

Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial atakuwa huru kuondoka Manchester United katika dirisha la usajili la Januari. Mchezaji huyo wa miaka 25 yuko huru kukaa katika Ligi ya Premia lakini anaweza kutafuta fursa barani, na Barcelona inaweza kuwa chaguo (Eurosport)

Mlinda mlango wa Manchester United na England Dean Henderson, 24, anataka uhamisho wa mkopo katika dirisha la uhamisho la Januari. (Sun)

Chelsea wanaandaa ofa mpya za mkataba wa kiungo wa England Mason Mount, 22, kiungo wa Ufaransa N’Golo Kante, 30, na kiungo wa Italia 29, Jorginho. (Standard)

Chelsea walikuwa tayari kutoa euro milioni 100 (pauni milioni 86) kwa ajili ya mlinzi wa Paris St-Germain na mlinzi wa Brazil Marquinhos, 27, katika majira ya joto(RMC Sport – in French)

at

Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski anasema “sio lazima ajithibitishe katika ligi nyingine” baada ya kushinda tuzo la mfungaji wa mabao mengi Uropa kwa kufunga mabao 41 ya Bundesliga na Bayern Munich msimu wa 2020-21. (Mirror)

Manchester City wanafuatilia fowadi wa Real Sociedad na Uhispania Mikel Oyarzabal, 24(TeamTalk)

Arsenal itamfanya kipa wa Ujerumani Bernd Leno, 29, apatikane kwa uhamisho kufuatia kuwasili majira ya kiangazi kwa kipa wa Uingereza 23 Ramsdale. (Eurosport)

Barcelona wanajiandaa kuachana na kocha mkuu Ronald Koeman, huku bosi wa Ubelgiji Roberto Martinez akiwa “chaguo bora” kuchukua nafasi ya Mholanzi huyo. (Goal)

p

Walakini, rais wa Barcelona Joan Laporta hajakata tamaa kujaribu kumshawishi bosi wa Manchester City Pep Guardiola arejee Nou Camp. Guardiola, 50, aliongoza Barca kushinda mataji matatu ya ligi ya Uhispania na Ligi mbili za Mabingwa wakati wa kipindi chake cha miaka minne akiwa usukani kati ya 2008 na 2012(El Nacional – in Spanish)

Winga wa Uhispania Marco Asensio, 25, anaweza kuondoka Real Madrid ikiwa hatapewa nafasi zaidi za kikosi cha kwanza chini ya Carlo Ancelotti msimu huu(Cadena Ser – in Spanish)

Kiungo wa Ureno Joao Palhinha, 26, yuko tayari kupandishwa mshahara huko Sporting Lisbon akihusishwa na kuhamia Everton, Tottenham na Wolves msimu huu wa joto. . (A Bola – in Portuguese)

Kiungo wa kati wa England wa Huddersfield Lewis O’Brien, 22, amekubali masharti ya mkataba mpya na Terriers licha ya ofa nne kutoka kwa Leeds United ya Ligi Kuu. (Football Insider)

Mlinda mlango wa Ajax na Cameroun Andre Onana, 25, anavutia nia kutoka Inter Milan na Napoli(Calciomercato – in Italian)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu