Naibu wa rais nchini Kenya amesema kwamba Wakenya watajiamulia kuhusu mgogoro wa kisiasa kati yake na rais Uhuru Kenyatta.
Kwa takriban miaka minne sasa, uhusiano kati ya naibu huyo William Ruto na rais Uhuru Kenyatta umekuwa mbaya.
Bwana Ruto anamtuhumu rais Kenyatta kwa kubadilisha ajenda ya serikali baada ya kukutana na aliyekuwa mpinzani wake mkuu Raila Odinga katika kile kinachoitwa Handshake.
Hivi majuzi katika mkutano wa eneo la Sagana, a Rais Uhuru Kenyatta ambaye alikuwa akikutana na watu wa jamii yake kutoka mlima Kenya alisema kwamba alimfahamisha bwana Ruto yote yaliokuwa yakiendelea kabla ya Handshake yake na Raila Odinga licha ya naibu huyo kudai kwamba hakaufahamu kilichokuwa kikiendelea.
Rais Uhuru Kenyatta ameamua kumuunga mkono mpinzani wake wa siku nyingi Raila Odinga badala ya naibu wake William Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
