Venezuela kutoa mapipa milioni 50 ya mafuta kwa Marekani baada ya Maduro kuondolewa Madarakani

In Kimataifa

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Venezuela itatoa mapipa milioni 30 hadi 50 ya mafuta kwa Marekani, kufuatia operesheni ya kijeshi iliyomuondoa Rais Nicolás Maduro madarakani.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump alisema mafuta hayo yatakuwa ya ubora wa juu na yatauzwa kwa bei ya soko. Aliongeza kuwa mapato yatadhibitiwa na yeye binafsi kwa madhumuni ya kuwanufaisha wananchi wa Venezuela na Marekani.

Tamko hilo linakuja wakati Trump akidokeza kuwa sekta ya mafuta ya Marekani itaanza kufanya kazi nchini Venezuela ndani ya miezi 18, huku akitabiri uwekezaji mkubwa katika nchi hiyo. Hata hivyo, wachambuzi wanasema kurejesha uzalishaji wa mafuta wa Venezuela kwa viwango vya awali kunaweza kugharimu mabilioni ya dola na kuchukua hadi muongo mmoja.

Kauli ya Trump imetolewa siku moja baada ya Delcy Rodríguez kuapishwa kuwa rais wa mpito wa Venezuela. Rais wa zamani Nicolás Maduro yuko nchini Marekani akijibu mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya na umiliki haramu wa silaha.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Rais Samia aweka shada Kaburi la Mashujaa Urusi

Rais Samia Suluhu Hassan leo ameweka shada la maua katika Kaburi la Mashujaa jijini Moscow Urusi kwa heshima ya

Read More...

JKT yawaita wahitimu Form 6 2026 kujiunga na mafunzo ya lazima

Jeshi la Kujenga Taifa limewataka vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2026 kutoka shule zote za Tanzania

Read More...

Arsenal Hatimaye Watwaa Taji la Premier League Baada ya Miaka 22 ya KusubiriNa Semio Sonyo – Radio 5

Klabu ya Arsenal hatimaye imeandika historia mpya kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England (Premier League) baada ya kusubiri

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu