Wafanyakazi wa wapatao 51 wa kujitolea kutoka Taasisi ya Marekani ya Peace Corps wamekula kiapo cha utumishi wa kujitolea kwa muda miaka miwili nchini Tanzania katika sekta za afya na kilimo katika wilaya ishirini zikiwemo Iringa, Mufindi, Kondoa,Mbinga na Masasi.
Katika Hotuba yake jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwaapisha Kaimu Balozi wa Marekani nchini Vincent Spera, amesema dhamira ya wafanyakazi hao kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani pamoja na kusaidia jitihada za kimaendeleo za watanzania kwenye sekta mbalimbali.
Baadhi ya wafanyakazi wa kujitolea,wameelezea matuimaini yao ya kufanya kazi kwenye maeneo ambayo watapangiwa kwa kipindi hicho cha miaka miwili huku wakiahidi kufanya kazi hiyo kwa bidii hususan kwenye maeneo ya vijijini ambayo yanakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma za afya.
Taasisi ya Peace Corps ni Serikali ya Marekani ambayo iliyoanzishwa na Rais John F. Kennedy mwaka 1961 hivi sasa ikiwa na zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea wapatao Elfu themanini kwenye takriban nchi 60 duniani
