WAHASIBU WA MALIASILI NA UTALII WAKUTANA ARUSHA

In Kitaifa, Uchumi

Wahasibu wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi, nidhamu na kuzingatia taaluma kwa kuwa wao ni walinzi wakuu wa nidhamu ya matumizi ya fedha za umma.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika Ufunguzi wa Kikao kazi cha Wahasibu wa Wizara na Taasisi zake Jijini Arusha Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bwana Nkoba Mabula amesema ubora wa taarifa za fedha zinazotolewa na wahasibu hao huathiri moja kwa moja uwajibikaji na taswira ya wizara mbele ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serrikali, Bunge na Wananchi.

Ameongeza kuwa kumekuwa na usimamizi mzuri wa fedha zote za Wizara na Taasisi, jambo lililowezesha Wizara kupata Hati safi ya CAG kwa miaka mitatu mfululizo ikiwa ni matokeo ya ushauri wa kitaalamu wa Wahasibu.

Ametaka kila Mhasibu kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia uadilifu, weledi na kuzingatia sheria na taratibu za fedha za Umma.

Aidha ndugu Mabula amewataka wahasibu hao kutumia kikao kazi hicho kama jukwaa la kujifunza, kubadilishana uzoefu na kujenga mshikamano wa kitaaluma ili kuongeza ufanisi wa usimamizi wa fedha za ummma katika wizara na taasisi zake.

Akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Mhasibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii, CPA Paul Kabale amesema lengo la kikao kazi hicho ni kuimarisha uwezo wa kitaaluma na kiutendaji wa Wahasibu ili kuhakikisha majukumu ya kifedha katika wizara ya maliasili na utalii na Taasisi zake yanatekelezwa kwa uwazi kwa kuzingatia sheria, Kanuni na Taratibu za fedha.

Aidha Ndugu Kabale amemhakikishia Naibu katibu Mkuu kuwa washiriki watafanya bidii katika kufuatilia mafunzo na kwa imani yake kuwa baada ya mafunzo, Wahasibu watakuwa tayari kuyaweka mafunzo hayo kwa vitendo katika utendaji yetu ya kila siku.

Kikao hiki cha siku mbili kimealika wakufunzi mbalimbali toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wizara ya fedha na wataalamu toka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambapo watapata mafunzo mtambuka ya Afya ya Akili kutoka kwa Mtaalamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Tanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Serikali za Tanzania na Serikali ya Marekani zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya afya ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu