Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewaapisha Wabunge wanne wa Chama cha Mapinduzi CCM.
Wabunge hao ni Pauline Gekul(Babati Mjini), James Ole Millya (Simanjiro), Joseph Michael Mkundi(Ukerewe) na Ryoba Marwa(Serengeti) ambao walipita katika majimbo yao bila kupingwa.
Wabunge wa Upinzani walisusia uapisho huo hawakuwepo bungeni wakati wabunge hao wakiapishwa.Wabunge hao wote walikuwa Wabunge kupitia tiketi ya CHADEMA kabla ya kuhamia CCM ambapo walipitishwa na kugombea nafasi hizo.
Baada ya kumaliza kuapishwa wabunge wa Upinzani walirejea Bungeni.



