Wasiopeleka michango ya wafanyakazi kushugulikiwa.

In Kitaifa

Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson ameiagiza Serikali kuchukua
hatua kwa waajiri wasiopeleka michango ya wafanyakazi katika
mifuko ya hifadhi ili kuondoa usumbufu kwa wastaafu wakati
wanapofuatilia stahiki zao.


Dk Tulia ameyasema hayo leo Jumatatu Juni 19 2023 wakati wa
kipindi cha maswali na majibu bungeni.


Agizo hilo lilitokana na majibu ya Naibu Waziri katika Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Patrobas
Katambi, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu,
(CCM) Angelina Malembeka.


Malembeka alihoji Serikali imejipangaje katika kuhakikisha
kuwa wastaafu wanapata mafao yao kwa wakati ikiwemo
wastaafu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).


Kutokana na suala hilo pia naibu Waziri Patrobas Katambi
akatoa namba ya simu ambayo wote wenye malalamiko juu ya
mafao na michango yao kutowasilishwa ili wanaweza kuitumia
kuwasiliana na Wizara (0715 939902).

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu