Serikali imesema kuwa inatarajia kuanza kutoa mikopo kwa
wanafunzi wa vyuo vya kati,kama ilivyosomwa katika bajeti ya
mwaka wa fedha 2023/24.
Hayo yameelezwa Bungeni leo na naibu wa Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolijia Omary Kipanga alipokuwa akijibu Swali
la msingi na lile la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum CCM
Dkt Thea Medadi Ntara.



