Bunge limeendelea na vuikao vyake jijini Dodoma ambapo
wabunge wameendelea kuchangia katika bajeti kuu ya serikali
2023/2024.
Moja ya mbunge aliyepata nafasi ya kutoa mawazo yake leo ni
mbunge wa jimbo la Magu Boniventura Kiswaga alichangia na
kueleza kuwa kama wapo waliomshauri waziri wa fedha katika
suala la kupunguza kodi ya mafuta ya kula yanayotoka nje na
kuongeza VAT kwa mafuta yanayozalishwa ndani hawamshauri
vizuri na kutishia kushika shilingi katika mshahara wake kama
hatobadili hilo.



