Bunge la Bajeti Limeanza leo, haya ndiyo ya msingi kufanyika

In Kitaifa

MKUTANO wa saba wa Bajeti wa Bunge la 11 umeanza leo mjini Dodoma ambao Juni 15 mwaka huu utapokea Taarifa ya Hali ya Uchumi na baadaye jioni Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Bunge jana, Mkutano huo wa Bunge la Bajeti utamalizika Juni 30, mwaka huu, na kwa kuanzia leo, utafanya kazi ya kumwapisha Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete na kisha kuwachagua wabunge tisa wa kuiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Aidha, kutakuwa na majumuisho kati ya serikali na Kamati ya Bajeti. Kesho Bunge mbali ya Kipindi cha Maswali na Majibu, pia serikali na Kamati ya Bajeti wataendelea na mashauriano na baadaye Kamati ya Uongozi itapokea taarifa ya Kamati ya Bajeti na Mashauriano ya Serikali.

Ratiba hiyo inaonesha kuwa bajeti za kisekta zitaanza Alhamisi wiki hii, kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuwasilisha, ambapo baada ya kuwasilishwa itajadiliwa kwa siku tano hadi Aprili 13, mwaka huu kabla ya Bunge kuingia katika mapumziko ya Ijumaa Kuu, Jumapili ya Pasaka na Jumatatu ya Pasaka.

Baada ya mapumziko hayo, Ofisi ya Rais ambayo ina wizara mbili za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itawasilisha bajeti yake Aprili 18 ambayo itajadiliwa hadi Aprili 21, mwaka huu.

Ofisi ya Makamu wa Rais zamu yake itakuwa Aprili 24 ikihusisha masuala ya Muungano na Mazingira, na siku inayofuata itakuwa zamu ya Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria itakayofuatiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano baada ya Sikukuu ya Muungano, na itaendelea baada ya Sikukuu ya Mei Mosi.

Mei 3, itakuwa zamu ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa siku mbili, kisha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa siku mbili, Mei 5 na Mei 8, mwaka huu, kabla ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itakuwa Mei 9, mwaka huu kwa siku moja.

Bajeti zitakazofuata baada ya hapo kwa mtiririko ni Maji na Umwagiliaji, Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi; Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; Viwanda, Biashara na Uwekezaji; Kilimo, Mifugo na Uvuvi; Maliasili na Utalii; Nishati na Madini; Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Fedha na Mipango itakamilisha bajeti za kisekta Juni 5 na 6, mwaka huu.

Kuanzia Juni 7 hadi 9, mwaka huu, serikali kwa kushauriana na Kamati ya Bajeti watafanya majumuisho kuzingatia hoja zenye maslahi kwa Taifa zilizojitokeza wakati wa kujadili Bajeti za Wizara; kabla ya Dk Philip Mpango kuwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi na Bajeti ya Serikali, Juni 15, mwaka huu. Bajeti itajadiliwa kwa siku saba kuanzia Juni 17 hadi Juni 24, mwaka huu itakapopitishwa kwa kura za wabunge.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Tigo na mjasiriamali Boss yaja kukomboa wajasiriamali

Katika kuendelea kukuza utalii wa utamaduni hapa nchini kampuni ya Tigo kanda ya kaskazini imeendeleaa kuwaunga mkono wadau wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu