Serengeti Boys yawatunishia Misuli Ghana

In Michezo

Wakati Timu soka ya Vijana chini ya Miaka 17, Serengeti Boys ikiwa inajiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana wa umri wao inayotarajiwa kufanyika Gabon mwezi ujao, Jana Serengeti Boys waliingia Kukipepeta na Team ya Ghana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar- Es-Salaam.

Serengeti Boys iliwatunishia Misuli Ghana na Kulazimishia Matokeo ya Kipenga cha Mwisho kuwa  2-2

Muhsin Malima ndiye aliyefunga bao la pili la kusawazisha kwa Serengeti Boys katika dakika za majeruhi baada ya mashabiki waliokusanyika uwanjani hapo wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kukata tamaa wakidhani mechi hiyo ingeisha kwa 2-1.

Ghana ilipata bao la kuongoza katika dakika ya 22 tu ya mchezo huo likifungwa na Sulley Ibrahim baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Serengeti Boys na kuuokokota mpira nje ya 18 na kupiga shuti lililojaa wavuni.

Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha vijana wa Serengeti ambapo dakika ya 35 Abdallah Rashid alifanya shambulizi la nguvu lakini akiwa na kipa akashindwa kufunga na mpira ukawahiwa na mabeki wa Ghana.

Serengeti haikuanza vizuri kipindi cha pili kwani sasa ilionekana kufa sehemu ya kiungo na kuruhusu wapinzani wao kuwapita kirahisi na katika dakika ya 76 Ghana waliandika bao la pili mfungaji akiwa Arko Mensah kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja langoni mwa Serengeti.

Dakika ya 90, Assad Juma aliisawazishia Serengeti bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti iliyotolewa na mwamuzi Elly Sasii baada ya mchezaji wa Ghana, Antah Isaac kushika mpira eneo la hatari.

Baada ya kusawazisha bao hilo Serengeti walibadilika na kulisakama lango la Ghana na zikiwa zimesalia dakika chache kabla ya mechi kumalizika ndipo Malima aliposawazisha bao la pili baada ya kuunganisha krosi nzuri ya Ibrahim Abdallah.

Hiyo ilikuwa mechi ya tatu ya kujipima nguvu kwa Serengeti baada ya kuifunga Burundi mabao 5-0 katika mechi mbili, ya kwanza 3-0 na ya pili 2-0.

Serengeti inatarajiwa kuondoka kesho kwenda Morocco kwa kambi ya mwezi mmoja kabla ya kwenda Gabon kwenye michuano hiyo ambayo Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza.

Serengeti inao uwezo wa kufuzu fainali za kombe la dunia kwa vijana zitakazofanyika India Novemba mwaka huu, ikiwa tu itafanikiwa kucheza nusu fainali za michuano hiyo ya Afrika.

Awali kabla ya mechi hiyo Waziri Mwakyembe alikabidhi bendera kwa timu hiyo na kuwataka kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika.

“Mmekabidhiwa bendera kwa niaba ya watanzania zaidi milioni 45, hivyo muende kutetea na kupigania bendera ya nchi yenu… serikali ina imani nanyi na iko pamoja nanyi,” alisema.

Akipokea bendera hiyo nahodha wa Serengeti Boys, Ally Msengi aliahidi kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Tigo na mjasiriamali Boss yaja kukomboa wajasiriamali

Katika kuendelea kukuza utalii wa utamaduni hapa nchini kampuni ya Tigo kanda ya kaskazini imeendeleaa kuwaunga mkono wadau wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu