Deontay Wilder: Anthony Joshua haniwezi.

In Kimataifa, Michezo

Bingwa wa ndondi katika uzani wa WBC Deontay Wilder anasema kuwa atampiga Anthony Joshua nyumbani kwake Uingereza.

Wilder mwenye umri wa miaka 32 alitetea taji lake dhidi ya Bermaine Stiverne siku ya Jumamosi , wiki moja baada ya Joshua kuhifadhi taji lake la ukanda wa WBA na IBF dhidi ya Carlos Takam mjini Cardiff.

”Viwanja vilivyojaa watu vinaonekana vizuri lakini Mecca ya ndondi ipo Marekani”, Wilder aliambia BBC Sport.

”Lakini kama unataka kusalia nyumbani kama msichana mdogo mfalme huyu hajali kuja na kumwangusha bingwa”.Katika mahojiano na BBC Radio 5, Wilder alimshutumu promota Eddie Hearn kwa kuwadanganya mashabiki kwamba Joshua ndio bondia bora katika uzani mzito duniani.

”Iwapo Joshua ndio bora, na bingwa , Waingereza wanafaa kumwambia ajitokeze na apigane ndio mujue kwamba yeye ndio bora”.

”Moyo wangu unaniambia kwamba mimi ndio bora na kama sio bora basi ningependa aliye bora aje anionyeshe”

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu