Mbwana Samatta kuikosa Benin.

In Kimataifa, Michezo

Wakati shirikisho la soka nchini TFF likiendelea kutangaza kuwa na uhakika wa kumtumia mshambuliaji wa klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta katika mchezo wa Taifa Stars, imeelezwa kuwa mshambuliaji huyo ambaye ni nahodha wa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, atakaa nje kwa majuma sita akiuguza majeraha ya goti.

 

TFF kupitia kwa afisa habari wake Alfred Lucas, leo mchana ameviambia vyombo vya habari kuwa, mshambuliaji huyo atajiunga na kikosi cha Taifa Stars mjini Benin tayari kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa mwishoni mwa juma hili.

 

Lakini taarifa za kuumia kwa Samatta zinadhihirisha hatokua sehemu ya kikosi Tanzania katika mchezo huo.

 

Samatta aliumia goti mwishoni mwa juma lililopita, wakati akiichezea Genk dhidi ya Lokeren na kulazimika kutolewa nje katika dakika ya 40.

 

Samatta ameonekana kupata maumivu katika goti lake katika misuli na mifupa miepesi, ambayo kitaalamu inajulikana kama Meniscus.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu