Kikao kazi cha serikali mtandao chaanza jijini Arusha

In Kitaifa

Kikao kazi cha Serikali Mtandao kitachofanyika kwa siku tatu, kimeanza leo katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano AICC Jijini Arusha,kikihusisha Maafisa Masuuuli,Maafisa Tehama na watumiaji wote wa mifumo ya Tehama Serikalini.

Mkutano huo amabao umeambatana na maadhimisho ya miaka kumi ya Mamlaka ya serikali Mtandao,na una kauli mbiu isemayo Mifumo Jumuishi ya TEHAMA kwa utoaji Bora wa Huduma kwa Umma.

Mkutano huo umehudhuriwa na washiriki zaidi ya elfu moja wakiwemo Wadau wa Tehama na viongozi mbali mbali wa serikali, Viongozi wa dini na wanahabari.

Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi IGA Dkt Mussa Kissaka,katika hotuba yake akabainisha baadhi ya Malengo yaliyowekwa na bodi hiyo kwa kipindi cha miaka kumi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt Laurean Ndumbaro, amewataka viongozi wa serikali na Taasisi zake ambao bado hawajaanza kutumia mfumo huo wa TEHAMA,kufanya hivyo ili kuleta maana kamili ya Serikali kuwa ya mtandao.

Nae Mgeni Rasmi katika mkutano huo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deo Ndejembi aliyemwakilisha Waziri Jenista Mhagama katika hotuba yake,licha ya mengi aliyozungumza amezisisitiza Taasisi za serikali na za Binafsi kutumia mfumo wa TEHAMA ili kuweza kurahisisha kazi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu