Wanasema Ukiachana na Mpenzi wako halafu ukarudiana naye, Mkaachana tena halafu Mkarudiana kwa mara ya Pili, Basi Mjue huo utakuwa Utamaduni wenu.
Mfano mzuri umekuwa kwa Wapenzi Wawili, Rapper Tyga naMwanadada kutoka Familia ya Kardashian, Kylie Jenner.

Taarifa mpya Mjini ni kwamba Tyga na Mpenzi wake Kylie Wameachana kwa mra nyingine tena ikiwa ni mara ya tatu.
Mtandao wa People umeeleza kwa kunukuu taarifa zilizotoka kwenye Chanzo cha Karibu na Couple hiyo ambacho Kimelithibitisha hilo lakini chanzo chenyewe kikasema kwamba imekuwa ni kawaida yao kupeana Likizo ya Mapenzi na Kurudiana na hivyo huenda Watayamaliza na kurudiana tena.
“They tend to take little breaks all the time and then get back together. It’s definitely possible they’ll work things out again,” —kilisema chanzo hicho.
Tyga na Kylie wao wamekuwa watu wa Mapenzi ya ON & OFF, Sababu kubwa ikiwa ile inayosemekana kwamba Familia ya Kardashian inakuwa na Maamuzi ya Mahusiano ya Watoto Wao sometimes kitu ambacho kinafanya Muda mwingine Mtoto wa Kike kukosa nguvu ya Kulitetea penzi lake kwa Mwanaume ampendaye.
