Mazishi ya Mwanasiasa mkongwe nchini Balozi Job Lusinde(90) ambaye alikuwa mmoja wa baraza la kwanza la mawaziri la Mwalimu Julius Nyerere baada ya uhuru,yatafanyika kesho eneo la Chikulu jijini Dodoma alipotaka azikwe.
Balozi Job Lusinde alifariki dunia juzi Julai 7 2020 jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.
Ndiye alikuwa Waziri mdogo kuliko wote katika Baraza la Kwanza la Mawaziri la Tanganyika na ndiye amekuwa wa mwisho kufariki kwani wenzake wote walishatangulia mbele za haki.
