Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imesisitiza kuwa
mitaala ya Elimu ya Msingi na Sekondari imeweka bayana
muda unaopaswa wanafunzi kusoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda
amesema kuwa mtaala wa Elimu ya Msingi unaeleza kuwa
muda wa kusoma Elimu ya Awali na Darasa la kwanza hadi la
pili ni saa tatu (dakika 180) tu kwa siku.
Kila kipindi kimoja Waziri ameongeza, kipindi kimoja ni dakika
30.
Prof Mkenda ameongeza kuwa muda wa kusoma kwa darasa la
tatu hadi la saba ni saa sita (dakika 360) kwa siku na kila kipindi
ni dakika 40.
Kwa upande wa Elimu ya Sekondari muda wa kusoma ni saa 5
na dakika 20 na kipindi kimoja ni dakika 40.
Waziri Mkenda ametoa maelezo hayo Bungeni, Dodoma leo
Jumanne, baada ya Mbunge wa Viti Maalum Ng’wasi Kamani
kutaka kufahamu endapo Serikali imeweka katika sheria ukomo
wa saa za kufundishwa wanafunzi kama ilivyoweka kisheria
ukomo wa saa za kufanya kazi kwa waajiriwa.
